Sunday, July 19, 2015

IFAHAMU BIASHARA YA MTANDAO ITABADILI MAISHA YAKO. NETWORK MARKETING( BIASHARA YA MTANDAO ).


Hii biashara ilianza mwanzoni mwa karne ya ishirini miaka ya 1920s huko Marekani kupitia kiwanda kimoja kilichokuwa kikijihusisha na utengenezaji wa virutubisho vya mwili,kiwanda hicho kilianzisha mfumo wa kuwalipa fidia wateja waliokuwa wakizinunua bidhaa zao,pia iliwalipa watu waliofanikiwa kuwaingiza watu wapya katika mtandao wa ununuaji na usambazaji wa bidhaa za kiwanda hicho.Kupitia mfumo huu kiwanda hicho kiliweza kukua kwa kasi sana kitu kilichosababisha wafanya biashara wakubwa wengine wajiunge na mfumo huu na kufungua makampuni mbalimbali yaliyoanza kufanya biashara kwa kutumia mfumo huu.Mpaka sasa hivi karibia watu laki moja wanajiunga na mfumo huu wa biashara kila wiki nchini marekani,na zaidi ya watu milioni mia tisa kumi na tano wanafanya na hii biashara duniani kote

BIASHARA HII NI NINI HASA!!!!!!!

Biashara hii kama nilivyosema hapo mwanzo ni mfumo wa biashara ambao mbali na kumlipa mwanachama (member) wa kampuni pindi anunuapo bidhaa kila mwezi,mwanachama huyo pia hulipwa aingizapo mwanachama mpya na pia hulipwa kila mwezi kutokana na manunuzi ya mwezi mzima.Hii inamaanisha kuwa mbali na mwanachama kujiingizia faida ya reja reja kupitia mauzo ya bidhaa anazonunua moja moja kutoka kiwandani pia atarudishiwa asilimia flani ya manunuzi yake (bonus) kila mwezi kulingana na jumla ya manunuzi yake kwa mwezi,pia kampuni itamlipa yeye akiwa kama ''upliner'' kwa manunuzi yatakayofanywa na wanachama aliofanikiwa kuwaingiza katika kampuni lake analofanya nalo biashara.
Wanayabiashara wengi duniani wanausapoti mfumo huu,watu kama kina Robert Kiyosaki,Michael Loise,Jim Rhon,,James Mang'amba na wengine wengi ni watu waliofanikiwa kupitia mfumo na kupitia biashara hii wanajiingizia mamilioni ya pesa kila mwezi,na wanatoa mafunzo mbali mbali kuhusiana na biashara hii.

FAIDA YA BIASHARA HII.

Kuna faida mbali mbali katika biashara hii ya mtandao lakini kwa leo nitaongelea faida chache tu za mhimu mtu anazoweza kuzipata kama ataamua kuifanya biashara hii.
1 :Utafanya biashara hii hata kama ukiwa nyumbani au mahali popote.
Biashara unaweza ifanaya ukiwa mahali popote hata kama ni nyumbani,ofisini au safarini.Unaweza ifanya kupitia simu yako au komputer yako kuwasiliana na wateja wako ,kutafuta wateja au kutangaza bidhaa zako,ndio maana wanasema biashara ya mtandao ni biashara ya karne ya ishirini na moja kwa sababu hii ni biashara inayotumia mfumo wa kisasa wa kiteknolojia,haihitaji mpaka ufungue duka au upeleke bidhaa sokoni,ofisi yako ni simu yako,computer au notebook.Pia haijalishi uwe ni mama wa nyumbani mwenye majukumu ya kulea familia au mwajiriwa wa ofisini unaweza ifanya kwa mda wowote unaokua huru kwa kutafuta wateja aukujenga team yako.
2 :Inakupatia vipato vitatu kwa wakati mmoja.
Unapofanya biashara hii unajiingizia vipato vya aina tatu kwa wakati mmoja.itakupatia kipato cha rejareja kwa bidhaa unazouza,pili itakupatia bonus za kila mwezi kulingana na jumla ya manunuzi yako na pia inakupatia bonus ya manunuzi ya team uliyotengeneza,biashara tulizozizoea zinaingiza kipato cha rejareja tu,ila hii inakupatia vyote hivi.Pia unaweza endelea jiingizia mshahara kutoka katika kazi uliyoajiriwa wakati ukiendelea jiingizia vipato hivyo vitatu kutoka katika hii biashara.
NOTE ;Kila company ina vigezo vyake katika kukulipa bonus,na kiwango cha malipo hivyo inakupasa kwanza kufanya uchunguzi na kufahamu ni kampuni gani inayokufaa. 
3 :Inakuingizia kipato hata kama unaumwa au upo likizo.
Utaweza jiingizia kipato hata kama unaumwa au upo likizo kupitia team uliyotengeneza.Hapa ndio faida kubwa katika hii biashara,ajira haina warrant unapougua mwajiri awezi kukuvumilia mwaka mzima,duka lako unapougua ukilifunga hakuna kipato chochote kitakachoingia,lakini hii biashara uugue au hata kama umeamua kwena likizo bado mfereji wa hela ulioutengeneza kupitia team yako utaendelea kukuingizia pesa,je ni kazi gani au biashara gani nyingine itakayokuingizia kipato hata kama haujatumia nguvu yako tofauti na hii?,ndio maana nakwambia ukifanya biashara ya mtandao unaweza kustafu hata kama bado kijana(una nguvu).
4 :Inakusaidia kuepuka makato ya kodi.
Katika ajira na biashara za kawaida unalipa kodi kulingana na mshahara au kipato unachoingiza kwa mwezi,mshahara ukiwa mkubwa na kodi inaongezeka,biashara ikiwa kubwa pia makato ya kodi yanakuwa makubwa.Hivyo ni vigumu kwa mfanya kazi kuhifadhi sehemu ya mshahara wake kwa ajiri ya maendeleo kutokana na makato na ni vigumu pia kuanzisha biashara ya duka kama huna uhakika mzunguko wa biashara utakuawa kama utakua mzuri kwa sababu TRA watakufirisi.Lakini katika hii biashara TRA utakua unawasikia kwenye redio kwani hawatakuhusu kabisa kupitia biashara hii,hii ni kwasababu bidhaa zako zinalipiwa kodi na kampuni unalofanya nalo kazi pindi zinaingia nchini hivyo hutapaswa tena kulipa kodi.
5 :Unaweza ianza biashara hii kwa mtaji mdogo kabisa.
Kila kampuni linalojihusisha na biashara ya mtandao lina utaratibu wake
wa gharama za kuanzia katika biashara hii.Hivyo ni jukumu lako kuangalia ni kampuni gani litakufaa kuanza nalo biashara kwa mtaji ulionao,lakini kitu cha msingi katika hii biashara mtaji wa kuanzia ni mdogo sana ukilinganisha na jinsi mtu anayetaka kufungua duka au biashara nyingine.Pia unauwezo wa kuukuza mtaji wako mpaka ukawa mkubwa kwa mda mfupi kulingana na malengo uliyojiwekea.
6 :Inakupa uwezo wa kuchagua ni watu gani unaohitaji kufanya nao kazi.
Biashara ya mtandao inakupa uwezo wa kuchagua watu unaowahitaji kufanya nao biashara yako,katika biashara hii utaweza kuwa huru kuchagua watu unaoona wanafaa katika biashara yako,hii itakupa nguvu ya kibiashara kwasababu utafaya kazi na watu ambao unaona wanakufaa.
7:Unapata mafanikio kupitia kuwawezesha wengine.
Je,ushawahi kupewa shukrani kwa kumpa mtu njia ya mafanikio?,je,ushawahi kuwa kioo ambacho watu wanatumia kujitathmini katika jamii yako?,na ushawahi kuwa furaha ya watu wanaokuzunguka?.Biashara hii itakuwezesha kuwa msaada kwa watu wote wanaohangaika kwa kukosa ajira,wanaolipwa mshahara mdogo,wanaopata mateso kazini na ambao wanafanya kazi ambazo hazikua ndoto zao,wote hawa utawasaidia kwa kuwapa hii fursa ili wafanikiwe wakati huo huo wakikufanya nawe ufanikiwe,inapendeza sana eeh!!!
Zipo faida nyingi sana zinazohusiana na hii biashara ila kwa leo ningependa niishie hapo,napenda kukukaribisha wewe uliyechoka maisha ya kuranda randa kutafuta kazi,unayefanya kazi katika mazingira ya mateso na wewe uliyechoka maisha ya kukaa nyumbani bila shughuri yeyote,karibu uyabadili maisha yako kwa kuongeza thamani katika jamii yako.Kwa msaada zaidi wasiliana nami BONIVENTURE JOACHIM kwa njia zifuatazo;

Simu /watsup
: 0768-308740
E-mail : bnjige@gmail.com

IF YOU DON'T TAKE RISK YOU WILL WORK FOR THOSE WHO TAKES IT.


Watu wengi huogopa kuchukua maamzi magumu ya kimaendeleo kwa sababu wanaogopa kushindwa au kupata hasara katika kufanikisha mambo wanayotamani kuyafanya au kuyapata..Huofia huenda wakapata hasara itakayopelekea kupoteza hata kile kidogo walichonacho na hivyo kubakia wakitamania mambo mazuri.
Katika dunia hii watu wote waliofanikiwa ni watu ambao waliamua kuthubutu kuyafanya yale waliokuwa wanataka wayafanye,watu hawa ndio walio fanikiwa na leo hii kila mtu anatamani mali na utajiri walio nao.Mfano mzuri ni kama vile ROBART KIYOSAKI,huyu ni mjasiriamali mkubwa duniani ambaye watu wengi wanayatamani mafanikio yake,kwa sasa kwa mwezi mmoja anaingiza karibia $ 2 MIlLIONS (dola milion mbili) ambazo kwa thamani ya kitanzania ni shilingi 3,400,000,000 (yaani bilioni tatu na milioni mia nne).Mbali na kutoka katika familia ya kisomi aliona kuwa elimu ya shule isinge msaidia katika kufanikisha ndoto zake hivyo aliamua kujiingiza katika biashara ambayo mara nyingi alifeli ila hakukata tamaa kwasababu hakuogopa kuthubutu.Leo hii anamiliki miradi mingi na mikubwa sehemu mbalimbali duniani na kaajili watu wengi wenye elimu zao.
Mafanikio yanawapata watu wanaothubutu kwani hao hawakuogopa kufeli hivyo kama wewe unaogopa kufeli huwezi kufanikiwa kwasababu huwezi kutubutu.Wasomi wengi kwa sasa wapo mtaani wakiangaika kutafuta kazi maofisini bila mafanikio na kubaki wakiulaumu mfumo mbaya wa serikali,kutokana na fikra zao potofu wanashindwa kuyatumia mazingira yanayowazunguka ili wajiajili wenyewe,katika hii dunia hata kama kama umezungukwa na mawe unaweza kuyageuza mawe kuwa raslimali yako na kukuingizia kipato,itategemea na wewe unayoyachukuliaje hayo mawe.Kama unamalengo ya kufanikiwa na kuwa na uhuru wa pesa hakuna kazi ya kuajiriwa itakayokupa uhuru wa pesa kulingana na mfumo wa dunia unaohusiana na ajira.
Kama unahitaji mafanikio na kuwa na uhuru wa pesa thubutu kufanya kile ambacho unatamani kukifanya leo bila kujarisha upo kazini,haupo kazini,umesoma,haujasoma kwa sababu mafanikio ya pesa yanatokana na jinsi ya wewe unavyoweza kuiwekeza pesa hata kama ni kidogo ili ije kujizalisha na sio wewe unaingiza shilingi ngapi kwa mwezi kwan hata kama unaingiza milioni moja kwa mwezi na matumizi yako ni laki tisa na nusu kwa mwezi huwezi fanana na anaeingiza shilingi laki tano na matumizi yake kwa mwezi ni laki mbili kwa mwezi.
Wekeza pesa yako sasa katika biashara ili uje uwe na uhuru wa pesa zitakazokufanya utimize ndoto zako kwa sababu kama ukiogopa kuthubutu utakuja kuwatumikia wale walioamua kuthubutu.

SCHOOL DID'NT TRAIN YOU TO BE BUSINESS OWNER IT TRAINED YOU TO BE IMPLOYED FOR RICH.


Hellow wapendwa natumaini wote mu wazima na kwa wale ambao hampo sawa poleni na naamini Mungu atawapa uponyaji.Siku ya leo nimependa tujifunze ni jinsi gani mfumo wa elimu ambavyo unatujenga tuwe wategemeaji kwa kutujenga kuja kuajiriwa na sio kujiajiri sisi wenyewe.
Katika mfumo wa elimu Tanzania na duniani kwa ujumla hakuana mtaala unaomjenga mtu kuja kujiajiri mwenyewe bali unamtengenezea mwanafunzi mazingira ya kuja kuajiriwa,kwa mfano,nilikutana na mwanafunzi aliyehtimu shahada ya kwanza biashara akilalamika katafuta kazi bila mafanikio,nilipomuuliza kwani huwezikwa kutumia elimu uliyonayo juu ya biashara kujiajiri mwenyewealidai tatizo ni mtaji.Hapo ndipo nilipogundua kumbe hata wanaosomea biashara wapo sawa kama waliosomea shahada nyingine.
Mfumo wa elimu haumfundishi mwanafunzi kuja kujiajiri bali unamfundisha mtu kuja kuwatumikia matjiri(wafanya biashara),kwa mfano unakuta mtu kasomea uhandisi ila kaajiriwa katika kampuni la uhandisi la mfanyabiashara aliyeishia form four,na anafurahia hiyo kazi kwa kuona analipwa kipato kikubwa bila kujua kwamba yeye anamuingizia mara themanini au tisini mwajiri wake.
SIku hizi wafanyabiashara wakubwa kama kina Bakhresa wanawatumia wasomi kwa kununua projects proposal mbali mbali na kuzifanyia kazi zinazowaingizia mabilioni ya pesa na unakuta aliyeiuza hiyo proposal anafurahia kisa amaelipwa milioni ishirini au thelasini.
Mafanikio ya mtu yanaangaliwa katika pesa na jinsi gani anatumia akili yake katika kukikuza kipato chake,hapa haijarishi kichwani kwako umebeba degree ngapi,unakuta mtu anapata fursa ya kufanya biashara anadai hawezi ichafua degree yake kwa kufanya biashara za kijinga wakati kina pinda na uwaziri wao wanawekeza mpaka mashambani ambapo ndio panaonekana pa walala hoi.Tumia elimu uliyonayo kukikuza kipato chako,hata kama unaajira usitegemee utakaa kwenye ajira miaka yote siku utakapoishiwa nguvu hajkuna atakayeangalia umesomea chuo gani wala nchi gani kwa sababu hautakua na faida yeyote,na kama unasubiria pensheni ndio ikutajirishe unajidanganya kwasababu nguvu unayoitumia inatengebneza mamilioni ya pesa kwa mwajiri wako na hiyo pesheni yako ni vijisenti tu katika rundo la pesa ulilotengeneza.
Kuanza biashara haijarishi una shilingi ngapi mfukoni kwani unaweza izalisha shilingi hamsini uliyonayo ikawa mia,elfu na mwisho wa siku ukawa mfanya biashara mkubwa,kuwa tajiri haijarishi kiasi kiasi kikubwa cha pesa unachotengeneza kwa mwezi bali unawekeza kiasi gani cha kipato chako katika miradi.

JE UNASUMBULIWA NA KISUKALI?


Miongoni mwa magonjwa sugu yanayoendelea kuathiri afya za mamilioni ya watu katika nchi nyingi duniani zikiwemo za bara la Afrika ni ugonjwa wa kisukari. Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni 285 wanasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari duniani ambapo karibu asilimia 90 ya wagonjwa hao wana aina ya pili ya kisukari. Jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa, idadi ya watu wenye kisukari inaongezeka kwa kasi na wataalamu wanasema kuwa, ifikapo mwaka 2030 idadi hiyo itaongezeka maradufu. Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wa kisukari katika nchi za Asia na Afrika, na inasemekana idadi hiyo inatokana na kukua miji na mabadiliko ya maisha ya watu katika nchi zinazoendele, na labda kutokana na kuiga mifumo ya maisha ya Kimagharib
Ugonjwa wa kisukari au Diabetes Mellitus hutokea pale tezi kongosho au pancrease inaposhindwa kutengeneza homoni au kichocheo aina ya Insulin, au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho cha insulin na kusababisha kuongezeka kiwango cha sukari kwenye damu au kitaalamu hyperglycemia. Insulin ni kichocheo au homoni inayotengenezwa na kongosho ili kudhibiti sukari katika damu. Ugonjwa wa kisukari unaweza kusababishwa kuwa na kiwango kidogo cha Insulin mwilini, mwili kutosikia kichocheo hicho au yote mawili.

Nimefanya utafiti kwenye Biblia kuhusu utajiri na umasikini; "case study" nimetumia tajiri wa kupindukia; Mzee Ibrahim na masikini wa kupindukia; Bw. Lazaro. Kuna mambo matatu nikagundua. Mosi, wote wawili walifanikiwa kuingia mbinguni. Kwa hiyo wanaojifariji kuwa "matajiri", hawaingii mbinguni, inabidi watambue kuwa wafanyabiashara na matajiri wakubwa wa kwenye Biblia wanakula "maisha" Mbinguni kwa raha zao; kuanzia Ibrahim, Akila, Mfalme Suleiman, Ayubu, Dorkasi na wengine kibao. Pili ni maisha waliyoishi (Ibrahim na Lazaro) duniani. Wakati Ibrahim alikuwa akila na kusaza; tunaambiwa Lazaro alikuwa "anagongea" makombo kwa yule tajiri. Kwa hiyo Ibrahim aliishi kwa "kutanua" duniani wakati Lazaro aliishi maisha ya "kupigika kinoma". Tatu ni walipofika Mbinguni. Tunaambiwa masikini alipumzishwa kifuani mwa Ibrahim. Kuna vipengele viwili nikaviona hapa. Cha kwanza ni kuwa mtu anaepumzishwa ni yule aliyechoka. Lazaro ni kweli aliingia mbinguni lakini akiwa amechoka na kupigika(kutokana na mateso ya umasikini wa duniani) Cha pili ni kwamba Ibrahim alipewa nafasi(kiti) Mbinguni lakini masikini Lazaro hakuwa na pa kukaa ndio maana ikabidi "agongee" kifuani mwa Ibrahim. Kwa hiyo nikagundua kwamba Lazaro aliishi kwa kupigika duniani na bado "akawa wa kugongea" Mbinguni. Wakati Ibrahim aliishi kwa "matanuzi duniani" na bado akaendelea "kujinafasi" Mbinguni. Baada ya hayo nikajiuliza, "nifanyeje?" Nikagundua tena kumbe Biblia ni kitabu cha machaguo; mbele yamewekwa mema na mabaya, unaloamua kuchagua ndilo unalolipata. Ukichagua U-Lazaro unakuwa Lazaro kwa tabu zako, ukichagua U-Ibrahim basi unajiwea Ibrahim kwa raha zako. Mimi nimeamua kuchagua U-Ibrahim; ijapokuwa uwe masikini ama tajiri kiuchumi, maadam unamjua Mungu na kuishi maisha ya utakatifu, Mbinguni utaingia.

IFAHAMU BIASHARA YA MTANDAO ITABADILI MAISHA YAKO. NETWORK MARKETING( BIASHARA YA MTANDAO ).


Hii biashara ilianza mwanzoni mwa karne ya ishirini miaka ya 1920s huko Marekani kupitia kiwanda kimoja kilichokuwa kikijihusisha na utengenezaji wa virutubisho vya mwili,kiwanda hicho kilianzisha mfumo wa kuwalipa fidia wateja waliokuwa wakizinunua bidhaa zao,pia iliwalipa watu waliofanikiwa kuwaingiza watu wapya katika mtandao wa ununuaji na usambazaji wa bidhaa za kiwanda hicho.Kupitia mfumo huu kiwanda hicho kiliweza kukua kwa kasi sana kitu kilichosababisha wafanya biashara wakubwa wengine wajiunge na mfumo huu na kufungua makampuni mbalimbali yaliyoanza kufanya biashara kwa kutumia mfumo huu.Mpaka sasa hivi karibia watu laki moja wanajiunga na mfumo huu wa biashara kila wiki nchini marekani,na zaidi ya watu milioni mia tisa kumi na tano wanafanya na hii biashara duniani kote.
BIASHARA HII NI NINI HASA!!!!!!!
Biashara hii kama nilivyosema hapo mwanzo ni mfumo wa biashara ambao mbali na kumlipa mwanachama (member) wa kampuni pindi anunuapo bidhaa kila mwezi,mwanachama huyo pia hulipwa aingizapo mwanachama mpya na pia hulipwa kila mwezi kutokana na manunuzi ya mwezi mzima.Hii inamaanisha kuwa mbali na mwanachama kujiingizia faida ya reja reja kupitia mauzo ya bidhaa anazonunua moja moja kutoka kiwandani pia atarudishiwa asilimia flani ya manunuzi yake (bonus) kila mwezi kulingana na jumla ya manunuzi yake kwa mwezi,pia kampuni itamlipa yeye akiwa kama ''upliner'' kwa manunuzi yatakayofanywa na wanachama aliofanikiwa kuwaingiza katika kampuni lake analofanya nalo biashara.
Wanayabiashara wengi duniani wanausapoti mfumo huu,watu kama kina Robert Kiyosaki,Michael Loise,Jim Rhon,,James Mang'amba na wengine wengi ni watu waliofanikiwa kupitia mfumo na kupitia biashara hii wanajiingizia mamilioni ya pesa kila mwezi,na wanatoa mafunzo mbali mbali kuhusiana na biashara hii.
FAIDA YA BIASHARA HII.
Kuna faida mbali mbali katika biashara hii ya mtandao lakini kwa leo nitaongelea faida chache tu za mhimu mtu anazoweza kuzipata kama ataamua kuifanya biashara hii.
1 :Utafanya biashara hii hata kama ukiwa nyumbani au mahali popote.
Biashara unaweza ifanaya ukiwa mahali popote hata kama ni nyumbani,ofisini au safarini.Unaweza ifanya kupitia simu yako au komputer yako kuwasiliana na wateja wako ,kutafuta wateja au kutangaza bidhaa zako,ndio maana wanasema biashara ya mtandao ni biashara ya karne ya ishirini na moja kwa sababu hii ni biashara inayotumia mfumo wa kisasa wa kiteknolojia,haihitaji mpaka ufungue duka au upeleke bidhaa sokoni.
2 :Inakupatia vipato vitatu kwa wakati mmoja.
Unapofanya biashara hii unajiingizia vipato vya aina tatu kwa wakati mmoja.itakupatia kipato cha rejareja kwa bidhaa unazouza,pili itakupatia bonus za kila mwezi kulingana na jumla ya manunuzi yako na pia inakupatia bonus ya manunuzi ya team uliyotengeneza,biashara tulizozizoea zinaingiza kipato cha rejareja tu,ila hii inakupatia vyote hivi.Pia unaweza endelea jiingizia mshahara kutoka katika kazi uliyoajiriwa wakati ukiendelea jiingizia vipato hivyo vitatu kutoka katika hii biashara.
3 :Inakuingizia kipato hata kama unaumwa au upo likizo.
Utaweza jiingizia kipato hata kama unaumwa au upo likizo kupitia team uliyotengeneza.Hapa ndio faida kubwa katika hii biashara,ajira haina warrant unapougua mwajiri awezi kukuvumilia mwaka mzima,duka lako unapougua ukilifunga hakuna kipato chochote kitakachoingia,lakini hii biashara uugue au hata kama umeamua kwengda likizo bado mfereji wa hela ulioutengeneza kupitia team yako utaendelea kukuingizia pesa.
4 :Inakusaidia kuepuka makato ya kodi.
Katika ajira na biashara za kawaida unalipa kodi kulingana na mshahara au kipato unachoingiza kwa mwaka,mshahara ukiwa mkubwa na kodi inaongezeka,biashara ikiwa kubwa pia kmakato ya kodi yanakuwa makubwa.Hivyo ni vigumu kwa mfanya kazi kuhifadhisehemu ya mshahara wake kwa ajiri ya maendeleo kutokana na makato na nivigumu pia kuanzisha biashara ya duka kama huna uhakika mzungukon utakuawa biashara utakua mzuri kwa sababu TRA watakufirisi.Lakini katika hii biashara TRA utakua unawasikia kwenye redio kwani hawatakuhusu kabisa kupitia biashara hii.
5 :Unaweza ianza biashara hii kwa mtaji mdogo kabisa.
Kila kampuni linalojihusisha na biashara ya mtandao lina utaratibu wake
wa gharama za kuanzia katika biashara hii.Hivyo ni jukumu lako kuangalia ni kampuni gani litakufaa kuanza nalo biashara kwa mtaji ulionao,lakini kitu cha msingi katika hii biashara mtaji wa kuanzia ni mdogo sana ukilinganisha na jinsi mtu anayetaka kufungua duka au biashara nyingine.Pia unauwezo wa kuukuza mtaji wako mpaka ukawa mkubwa kwa mda mfupi kulingana na malengo uliyojiwekea.
Zipo faida nyingi sana zinazohusiana na hii biashara ila kwa leo ningependa niishie hapo.

KUANZA BIASHARA TATIZO SIO MTAJI, FURSA POPOTE PALE ULIPO.


Hallow wapendwa,bila shaka mu wazima wa afya,kwa upande wangu mimi sipo vizuri sana kwani maradhi madogo madogo yananisumbua mimi pamoja na familia yangu,ila kiufupi tunamshukuru Mungu kwani bado anaendelea kutupatia pumzi yake.
Japokuwa nimebanana ila siku ya leo nimeona tujifunze somo hili la ni jinsi gani mtu unaweza kutumia fursa uliyonayo kuanza biashara na sio swala la mtaji.Tatizo la watu wengi hua ni kwamba anatamani kufanya biashara iliyokatika ndoto yake,biashara anayotaka kuifanya ni kubwa inayohitaji mtaji mkubwa na huo mtaji hana hivyo anabaki akisubiri mpaka pale atakapoupata huo mtaji ndio aanze biashara na wakati huo huo hajui huo mtaji ataupata leo,kesho,mwezi ujao au miaka mitano ijayo!!!!!,hivyo anabaki akisubiri mpaka siku hiyo ifike.
Swala la biashara ni swala ambalo kila mtu hua anatamani kulifanya,katika utafiti wangu mdogo nilioufanya,karibia 80% ya watu nilioongea nao wanandoto za kufanya biashara ila anasubiri mpaka pale mambo ya uchumi ykae sawa ndio aanze,huo ni uongo...,tena uongo mkubwa!!,katika uwanja wa biashara huwezi fanikiwa kama utakua na mawazo hayo,mtu anayeanza biashara kwa mtaji wa mdogo ni vyepesi sana kuwa billionare kama atajifunza biashara vizuri na akawa serious na biashara yake,mtu huyu akikaa kwenye biashara miaka mitano atamzidi yule atakayeanza biashara miaka mitano ijayo na akawa ana mtaji unaolingana na yule aliyeanza biashara miaka mitano iliyopita.Hii ni kwasababu huyu aliyeanza biashara kitambo atakua ashakabiliana na changamoto zote katika biashara na atakua anaelewa ni jinsi gani aendeshe biashara yake na kuzikwepa changamoto tofauti na huyo mpya ambaye kila kitu katika biashara kitakuwa kipya kwake.
Faida ya pili atakayoipata mtu anayeanza biashara kwa mtaji mdogo kwamba kadri atakavyozidi kufanya biashara ndio atapata ufumbuzi wa maswali mbalimbali aliyokua hayajui mwanzoni majibu yake na ataweza vumbua biashara mpya zenye faida kubwa kuliko ile aliyoanza nayo.Mimi niliishi na ndoto ya kufanya biashara tangu nikiwa mtoto,nikiwa mtoto nilisema nitafanya biashara nikiwa mkubwa,ila nilipokua nikagundua tatizo halikua umri nikajua kumbe unaweza kuwa mkubwa na bado ukashindwa kufanya biashara,hivyo nikagundua tatizo la watu wengi waliokua(yaani watu wazima) lipo katika mtaji,hivyo nikaanza kutafuta namna ya kuanza kukabiliana na njia gani nitaitumia kuweza kutatua tatizo la mtaji ili nianze biashara.Baada ya kuhangaika kutafuta ufumbuzi wa swali la mtaji lililokua linanisumbua nilikuja kufahamu kuwa tatizo la kuanza biashara sio mtaji ila ni jinsi ya kutafuta IDEA (WAZO) lililosahihi na kuligeuza kuwa biashara kulingana na hali ya kiuchumi utakayokua nayo kwa kipindi husika,hivyo mimi binafsi nilipata wazo la biashara lililoendana na hali ya uchumi niliyokua nayo na nikatengeneza biashara yangu iliyokua inaniingizia sihilingi hamsini Tsh. 50/= kwa kila bidhaa niliyokua naiuza,na ndio hapo nilipogundua kua hata hiyo faida ilikua ni kubwa sana na ingeweza kunifanya niifahamu biashara kwa undani zaidi na ndio ilivyokua.
Kitu kikubwa katika kuanza biashara ni kuangalia fursa gani inayokuzunguka katika jamii uliyopo ambayo inaweza kukuingizia faida yoyote,hapa usiangalie ni jamii gani inayokuzunguka kwani iwe kijijini,mjini,uswahilini,mtaa wa mashefa,iwe ni jamii ya vipofu au viziwi jamii yeyote ile unaweza fanya nayo biashara na ikauingizia faida kubwa (wanafunzi wengi wa vyuo wanaona hawawezi fanya biashara na wanafunzi wenzao kwasababu wanaona hawana pesa).Kitu kikubwa hapa ni kuwa mbunifu na kufanya biashara ambayo itakua tofauti kidogo na ile ambayo kila mtu anaikimbilia,mfano watu wengi wanakimbilia kufungua maduka na kuona ndio biashara pekee.
Katika ubunifu hapa ndio hua nasema ukiwa mbunifu unaweza tumia rasilimali yeyote inayokuzunguka hata kama ni mawe na ukajiingizia kipato,hapa nitauhusisha ule mfano wa story hii.
Mzungu mmoja alikua na mtaji wa shilingi Milioni moja na akataka kufanya biashara itakayompa faida kubwa (super normal profit) kwa kipindi kifupi.
Akaenda kwenye kijiji kimoja akawaambia wanakijiji ananunua Ngedere. So kila mwenye ngedere amletee atamnunua kwa sh.10,000/= kwa ngedere mmoja.
Wanakijiji wakachangamkia fursa. Wakakusanya ngedere kwenda kuuza kwa mzungu. Mzungu akanunua ngedere 50 kwa laki 5. Mara ngedere wakaisha.
Mzungu kuona ngedere wamepungua akapandisha dau. Ngedere mmoja sasa atamnunua kwa sh.15,000/=. Wanakijiji wajatafuta ngedere wakakosa. Akapandisha dau hadi 20,000/=.
Kwa tamaa ya fedha wanakijiji wakatafuta ngedere wakapata 20. Mzungu akalipa jumla ya sh.laki 4, yani 20,000/= kwa kila ngedere.
Mzungu akawa tayari amekusanya ngedere 70 na amebaki na laki moja. Akatangaza sasa atanunua ngedere kwa sh.30,000/= l, wanakijiji wakapagawa. Wakatafuta ngedere wakakosa. Mzungu akapandisha dau kuwa 40,000/= bado ngedere wakakosekana.
Sasa akafikisha dau la 50,000/= wanakijiji kwa tamaa ya fedha wakatafuta na wakafanikiwa kupata ngedere wawili. Mzungu akawanunua na kufikisha ngedere 72. By this time mtaji wa mzungu ulikua umeisha.
Lakini akazidi kutafuta ngedere. Sasa akapandisha dau kuwa 70,000/= kwa ngedere mmoja. Wanakijiji macho yakawatoka. Wakatafuta ngedere wakakosa.
Mzungu akapandisha dau kuwa 100,000/= kwa ngedere mmoja, wanakijiji mate yakawatoka. Tamaa ya fedha ikawakaba. Wakahangaika wee wakakosa ngedere hata mmoja.
Mzungu kuona hivyo akapandisha bei kuwa 150,000/= kwa ngedere mmoja lakini bado ngedere wakakosekana.
Akafikisha sh.200,000/= lakini hakupatikana ngedere hata mmoja. Sasa akaamua kupandisha bei hadi 300,000/= kwa ngedere mmoja.
Wanakijiji wakawaka tamaa. Kufikia hapa wakashindwa kuvumilia. Wakaamua kusaka ngedere kwa kwa udi na uvumba. Usiku na mchana.
Wakakesha msituni lakini hawakuambulia hata ngedere mmoja. Wakasikia kwenye kijiji cha jirani kuna mzee anauza ngedere. Wakaenda kijiji cha pili wakakuta ngedere wengi. Wakauliza bei, yule mzee akajibu ni laki mbili kwa kila ngedere.
Kwa kuwa yule mzungu aliwaambia atanunua kwa laki tatu wakaona ni biashara nzuri ikiwa watanunua kwa 200,000/= wakamuuzie yule mzungu kw 300,000/= watapata faida ya 100,000/= kwa kila ngedere.
Lakini hawakuwa na fedha. Wengine wakaaenda kukopa na wengine wakauza mali zao kama nyumba na ardhi ili wapate mtaji wa kufanya biashara ya ngedere.
Wakanunua ngedere wote kwa yule mzee, wakaenda nao kijijini. Sasa wakawa wanamngojea mzungu ili aje kununua kwao.
Wakasubiri siku ya kwanza hawakumuona, siku ya pili, ya 3, mara wiki, mara mwezi, mara mwaka... hawakuona mzungu wala Mchina.
U KNOW WHAT HAPPENED.
Wale ngedere waliokuwa kijiji cha pili ni wa yule mzungu. Alikua anawanunua kwa wale wanakiiji anakwenda kuwahifadhi kijiji cha jirani kw yule mzee.
Kichwani alijua kbs ipo siku ngedere wataisha na ataanza kuwauzia walewale wanakijiji bila wao kujua, tena atauza kwa bei kubwa.
Yeye alitumia milioni moja kununua ndedere 72.... sasa amekuja kuwauzia wanakijiji walewale kwa laki 2 kwa kila ngedere. Hivyo akapata jumla ya sh.milioni 14.4, Kisha akaondoka na hela zake, akawaachia wanakijiji ngedere wao plus madeni na umasikini wa kutupa.
Huo mfano unaonyesha ni jinsi gani unaweza kuwa mbunifu kwa kutumia fursa iliyopo katika jamii,ukaanza ukiwa na mtaji mdogo na mwisho wa siku ukawa milionnaire.Kikubwa ni kuwa mvumilivu,biashara zote ambazo zinaleta mafanikio watu wengi wanaziogopa ni ngumu mpaka uimudu na ianze kukuingizia faida kubwa inahitaji upitie mengi kwa kujifunza na kuimudu biashara (no gain without pain),biashara ni ngumu na inahitaji myo ndio maana hata wanaofanikiwa katika biashara ni wachache kama vile wanaoweza kukaa katika wokovu.
Anza kutumia fursa inayokuzunguka ili uwe wa kitofauti kwa kutengeneza maisha tofauti ambayo kila mtu atayatamani.
Asanteni kwa wote ambao mmefanikiwa kuisoma makala hii mpaka mwisho na naamini umejifunza kitu,kwa ulichojifunza usiende omba ushauri kwa mtu ambaye hana uelewa wa biashara,na hata kama ni mfanyabiashara sio mfanya biashara yeyote,hatakusaidia kwasababu hatakua na uelewa wa swala ulilomuuliza ila atatumia mawazo yake tu ambayo mwisho wa siku yatakukatisha tamaa,omba ushauri kwa mtu unayetamani kufanya nae biashara au kufanya biashara kama yake,huyu atakusaidia

Disqus Shortname

Comments system

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | coupon codes