Sunday, July 19, 2015

Nimefanya utafiti kwenye Biblia kuhusu utajiri na umasikini; "case study" nimetumia tajiri wa kupindukia; Mzee Ibrahim na masikini wa kupindukia; Bw. Lazaro. Kuna mambo matatu nikagundua. Mosi, wote wawili walifanikiwa kuingia mbinguni. Kwa hiyo wanaojifariji kuwa "matajiri", hawaingii mbinguni, inabidi watambue kuwa wafanyabiashara na matajiri wakubwa wa kwenye Biblia wanakula "maisha" Mbinguni kwa raha zao; kuanzia Ibrahim, Akila, Mfalme Suleiman, Ayubu, Dorkasi na wengine kibao. Pili ni maisha waliyoishi (Ibrahim na Lazaro) duniani. Wakati Ibrahim alikuwa akila na kusaza; tunaambiwa Lazaro alikuwa "anagongea" makombo kwa yule tajiri. Kwa hiyo Ibrahim aliishi kwa "kutanua" duniani wakati Lazaro aliishi maisha ya "kupigika kinoma". Tatu ni walipofika Mbinguni. Tunaambiwa masikini alipumzishwa kifuani mwa Ibrahim. Kuna vipengele viwili nikaviona hapa. Cha kwanza ni kuwa mtu anaepumzishwa ni yule aliyechoka. Lazaro ni kweli aliingia mbinguni lakini akiwa amechoka na kupigika(kutokana na mateso ya umasikini wa duniani) Cha pili ni kwamba Ibrahim alipewa nafasi(kiti) Mbinguni lakini masikini Lazaro hakuwa na pa kukaa ndio maana ikabidi "agongee" kifuani mwa Ibrahim. Kwa hiyo nikagundua kwamba Lazaro aliishi kwa kupigika duniani na bado "akawa wa kugongea" Mbinguni. Wakati Ibrahim aliishi kwa "matanuzi duniani" na bado akaendelea "kujinafasi" Mbinguni. Baada ya hayo nikajiuliza, "nifanyeje?" Nikagundua tena kumbe Biblia ni kitabu cha machaguo; mbele yamewekwa mema na mabaya, unaloamua kuchagua ndilo unalolipata. Ukichagua U-Lazaro unakuwa Lazaro kwa tabu zako, ukichagua U-Ibrahim basi unajiwea Ibrahim kwa raha zako. Mimi nimeamua kuchagua U-Ibrahim; ijapokuwa uwe masikini ama tajiri kiuchumi, maadam unamjua Mungu na kuishi maisha ya utakatifu, Mbinguni utaingia.

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments system

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | coupon codes