Hallow wapendwa,bila shaka mu wazima wa afya,kwa upande wangu mimi sipo vizuri sana kwani maradhi madogo madogo yananisumbua mimi pamoja na familia yangu,ila kiufupi tunamshukuru Mungu kwani bado anaendelea kutupatia pumzi yake.
Japokuwa nimebanana ila siku ya leo nimeona tujifunze somo hili la ni jinsi gani mtu unaweza kutumia fursa uliyonayo kuanza biashara na sio swala la mtaji.Tatizo la watu wengi hua ni kwamba anatamani kufanya biashara iliyokatika ndoto yake,biashara anayotaka kuifanya ni kubwa inayohitaji mtaji mkubwa na huo mtaji hana hivyo anabaki akisubiri mpaka pale atakapoupata huo mtaji ndio aanze biashara na wakati huo huo hajui huo mtaji ataupata leo,kesho,mwezi ujao au miaka mitano ijayo!!!!!,hivyo anabaki akisubiri mpaka siku hiyo ifike.
Swala la biashara ni swala ambalo kila mtu hua anatamani kulifanya,katika utafiti wangu mdogo nilioufanya,karibia 80% ya watu nilioongea nao wanandoto za kufanya biashara ila anasubiri mpaka pale mambo ya uchumi ykae sawa ndio aanze,huo ni uongo...,tena uongo mkubwa!!,katika uwanja wa biashara huwezi fanikiwa kama utakua na mawazo hayo,mtu anayeanza biashara kwa mtaji wa mdogo ni vyepesi sana kuwa billionare kama atajifunza biashara vizuri na akawa serious na biashara yake,mtu huyu akikaa kwenye biashara miaka mitano atamzidi yule atakayeanza biashara miaka mitano ijayo na akawa ana mtaji unaolingana na yule aliyeanza biashara miaka mitano iliyopita.Hii ni kwasababu huyu aliyeanza biashara kitambo atakua ashakabiliana na changamoto zote katika biashara na atakua anaelewa ni jinsi gani aendeshe biashara yake na kuzikwepa changamoto tofauti na huyo mpya ambaye kila kitu katika biashara kitakuwa kipya kwake.
Faida ya pili atakayoipata mtu anayeanza biashara kwa mtaji mdogo kwamba kadri atakavyozidi kufanya biashara ndio atapata ufumbuzi wa maswali mbalimbali aliyokua hayajui mwanzoni majibu yake na ataweza vumbua biashara mpya zenye faida kubwa kuliko ile aliyoanza nayo.Mimi niliishi na ndoto ya kufanya biashara tangu nikiwa mtoto,nikiwa mtoto nilisema nitafanya biashara nikiwa mkubwa,ila nilipokua nikagundua tatizo halikua umri nikajua kumbe unaweza kuwa mkubwa na bado ukashindwa kufanya biashara,hivyo nikagundua tatizo la watu wengi waliokua(yaani watu wazima) lipo katika mtaji,hivyo nikaanza kutafuta namna ya kuanza kukabiliana na njia gani nitaitumia kuweza kutatua tatizo la mtaji ili nianze biashara.Baada ya kuhangaika kutafuta ufumbuzi wa swali la mtaji lililokua linanisumbua nilikuja kufahamu kuwa tatizo la kuanza biashara sio mtaji ila ni jinsi ya kutafuta IDEA (WAZO) lililosahihi na kuligeuza kuwa biashara kulingana na hali ya kiuchumi utakayokua nayo kwa kipindi husika,hivyo mimi binafsi nilipata wazo la biashara lililoendana na hali ya uchumi niliyokua nayo na nikatengeneza biashara yangu iliyokua inaniingizia sihilingi hamsini Tsh. 50/= kwa kila bidhaa niliyokua naiuza,na ndio hapo nilipogundua kua hata hiyo faida ilikua ni kubwa sana na ingeweza kunifanya niifahamu biashara kwa undani zaidi na ndio ilivyokua.
Kitu kikubwa katika kuanza biashara ni kuangalia fursa gani inayokuzunguka katika jamii uliyopo ambayo inaweza kukuingizia faida yoyote,hapa usiangalie ni jamii gani inayokuzunguka kwani iwe kijijini,mjini,uswahilini,mtaa wa mashefa,iwe ni jamii ya vipofu au viziwi jamii yeyote ile unaweza fanya nayo biashara na ikauingizia faida kubwa (wanafunzi wengi wa vyuo wanaona hawawezi fanya biashara na wanafunzi wenzao kwasababu wanaona hawana pesa).Kitu kikubwa hapa ni kuwa mbunifu na kufanya biashara ambayo itakua tofauti kidogo na ile ambayo kila mtu anaikimbilia,mfano watu wengi wanakimbilia kufungua maduka na kuona ndio biashara pekee.
Katika ubunifu hapa ndio hua nasema ukiwa mbunifu unaweza tumia rasilimali yeyote inayokuzunguka hata kama ni mawe na ukajiingizia kipato,hapa nitauhusisha ule mfano wa story hii.
Mzungu mmoja alikua na mtaji wa shilingi Milioni moja na akataka kufanya biashara itakayompa faida kubwa (super normal profit) kwa kipindi kifupi.
Akaenda kwenye kijiji kimoja akawaambia wanakijiji ananunua Ngedere. So kila mwenye ngedere amletee atamnunua kwa sh.10,000/= kwa ngedere mmoja.
Wanakijiji wakachangamkia fursa. Wakakusanya ngedere kwenda kuuza kwa mzungu. Mzungu akanunua ngedere 50 kwa laki 5. Mara ngedere wakaisha.
Mzungu kuona ngedere wamepungua akapandisha dau. Ngedere mmoja sasa atamnunua kwa sh.15,000/=. Wanakijiji wajatafuta ngedere wakakosa. Akapandisha dau hadi 20,000/=.
Kwa tamaa ya fedha wanakijiji wakatafuta ngedere wakapata 20. Mzungu akalipa jumla ya sh.laki 4, yani 20,000/= kwa kila ngedere.
Mzungu akawa tayari amekusanya ngedere 70 na amebaki na laki moja. Akatangaza sasa atanunua ngedere kwa sh.30,000/= l, wanakijiji wakapagawa. Wakatafuta ngedere wakakosa. Mzungu akapandisha dau kuwa 40,000/= bado ngedere wakakosekana.
Sasa akafikisha dau la 50,000/= wanakijiji kwa tamaa ya fedha wakatafuta na wakafanikiwa kupata ngedere wawili. Mzungu akawanunua na kufikisha ngedere 72. By this time mtaji wa mzungu ulikua umeisha.
Lakini akazidi kutafuta ngedere. Sasa akapandisha dau kuwa 70,000/= kwa ngedere mmoja. Wanakijiji macho yakawatoka. Wakatafuta ngedere wakakosa.
Mzungu akapandisha dau kuwa 100,000/= kwa ngedere mmoja, wanakijiji mate yakawatoka. Tamaa ya fedha ikawakaba. Wakahangaika wee wakakosa ngedere hata mmoja.
Mzungu kuona hivyo akapandisha bei kuwa 150,000/= kwa ngedere mmoja lakini bado ngedere wakakosekana.
Akafikisha sh.200,000/= lakini hakupatikana ngedere hata mmoja. Sasa akaamua kupandisha bei hadi 300,000/= kwa ngedere mmoja.
Wanakijiji wakawaka tamaa. Kufikia hapa wakashindwa kuvumilia. Wakaamua kusaka ngedere kwa kwa udi na uvumba. Usiku na mchana.
Wakakesha msituni lakini hawakuambulia hata ngedere mmoja. Wakasikia kwenye kijiji cha jirani kuna mzee anauza ngedere. Wakaenda kijiji cha pili wakakuta ngedere wengi. Wakauliza bei, yule mzee akajibu ni laki mbili kwa kila ngedere.
Kwa kuwa yule mzungu aliwaambia atanunua kwa laki tatu wakaona ni biashara nzuri ikiwa watanunua kwa 200,000/= wakamuuzie yule mzungu kw 300,000/= watapata faida ya 100,000/= kwa kila ngedere.
Lakini hawakuwa na fedha. Wengine wakaaenda kukopa na wengine wakauza mali zao kama nyumba na ardhi ili wapate mtaji wa kufanya biashara ya ngedere.
Wakanunua ngedere wote kwa yule mzee, wakaenda nao kijijini. Sasa wakawa wanamngojea mzungu ili aje kununua kwao.
Wakasubiri siku ya kwanza hawakumuona, siku ya pili, ya 3, mara wiki, mara mwezi, mara mwaka... hawakuona mzungu wala Mchina.
U KNOW WHAT HAPPENED.
Wale ngedere waliokuwa kijiji cha pili ni wa yule mzungu. Alikua anawanunua kwa wale wanakiiji anakwenda kuwahifadhi kijiji cha jirani kw yule mzee.
Kichwani alijua kbs ipo siku ngedere wataisha na ataanza kuwauzia walewale wanakijiji bila wao kujua, tena atauza kwa bei kubwa.
Yeye alitumia milioni moja kununua ndedere 72.... sasa amekuja kuwauzia wanakijiji walewale kwa laki 2 kwa kila ngedere. Hivyo akapata jumla ya sh.milioni 14.4, Kisha akaondoka na hela zake, akawaachia wanakijiji ngedere wao plus madeni na umasikini wa kutupa.
Huo mfano unaonyesha ni jinsi gani unaweza kuwa mbunifu kwa kutumia fursa iliyopo katika jamii,ukaanza ukiwa na mtaji mdogo na mwisho wa siku ukawa milionnaire.Kikubwa ni kuwa mvumilivu,biashara zote ambazo zinaleta mafanikio watu wengi wanaziogopa ni ngumu mpaka uimudu na ianze kukuingizia faida kubwa inahitaji upitie mengi kwa kujifunza na kuimudu biashara (no gain without pain),biashara ni ngumu na inahitaji myo ndio maana hata wanaofanikiwa katika biashara ni wachache kama vile wanaoweza kukaa katika wokovu.
Anza kutumia fursa inayokuzunguka ili uwe wa kitofauti kwa kutengeneza maisha tofauti ambayo kila mtu atayatamani.
Asanteni kwa wote ambao mmefanikiwa kuisoma makala hii mpaka mwisho na naamini umejifunza kitu,kwa ulichojifunza usiende omba ushauri kwa mtu ambaye hana uelewa wa biashara,na hata kama ni mfanyabiashara sio mfanya biashara yeyote,hatakusaidia kwasababu hatakua na uelewa wa swala ulilomuuliza ila atatumia mawazo yake tu ambayo mwisho wa siku yatakukatisha tamaa,omba ushauri kwa mtu unayetamani kufanya nae biashara au kufanya biashara kama yake,huyu atakusaidia

0 comments:
Post a Comment