Sunday, July 19, 2015

IF YOU DON'T TAKE RISK YOU WILL WORK FOR THOSE WHO TAKES IT.


Watu wengi huogopa kuchukua maamzi magumu ya kimaendeleo kwa sababu wanaogopa kushindwa au kupata hasara katika kufanikisha mambo wanayotamani kuyafanya au kuyapata..Huofia huenda wakapata hasara itakayopelekea kupoteza hata kile kidogo walichonacho na hivyo kubakia wakitamania mambo mazuri.
Katika dunia hii watu wote waliofanikiwa ni watu ambao waliamua kuthubutu kuyafanya yale waliokuwa wanataka wayafanye,watu hawa ndio walio fanikiwa na leo hii kila mtu anatamani mali na utajiri walio nao.Mfano mzuri ni kama vile ROBART KIYOSAKI,huyu ni mjasiriamali mkubwa duniani ambaye watu wengi wanayatamani mafanikio yake,kwa sasa kwa mwezi mmoja anaingiza karibia $ 2 MIlLIONS (dola milion mbili) ambazo kwa thamani ya kitanzania ni shilingi 3,400,000,000 (yaani bilioni tatu na milioni mia nne).Mbali na kutoka katika familia ya kisomi aliona kuwa elimu ya shule isinge msaidia katika kufanikisha ndoto zake hivyo aliamua kujiingiza katika biashara ambayo mara nyingi alifeli ila hakukata tamaa kwasababu hakuogopa kuthubutu.Leo hii anamiliki miradi mingi na mikubwa sehemu mbalimbali duniani na kaajili watu wengi wenye elimu zao.
Mafanikio yanawapata watu wanaothubutu kwani hao hawakuogopa kufeli hivyo kama wewe unaogopa kufeli huwezi kufanikiwa kwasababu huwezi kutubutu.Wasomi wengi kwa sasa wapo mtaani wakiangaika kutafuta kazi maofisini bila mafanikio na kubaki wakiulaumu mfumo mbaya wa serikali,kutokana na fikra zao potofu wanashindwa kuyatumia mazingira yanayowazunguka ili wajiajili wenyewe,katika hii dunia hata kama kama umezungukwa na mawe unaweza kuyageuza mawe kuwa raslimali yako na kukuingizia kipato,itategemea na wewe unayoyachukuliaje hayo mawe.Kama unamalengo ya kufanikiwa na kuwa na uhuru wa pesa hakuna kazi ya kuajiriwa itakayokupa uhuru wa pesa kulingana na mfumo wa dunia unaohusiana na ajira.
Kama unahitaji mafanikio na kuwa na uhuru wa pesa thubutu kufanya kile ambacho unatamani kukifanya leo bila kujarisha upo kazini,haupo kazini,umesoma,haujasoma kwa sababu mafanikio ya pesa yanatokana na jinsi ya wewe unavyoweza kuiwekeza pesa hata kama ni kidogo ili ije kujizalisha na sio wewe unaingiza shilingi ngapi kwa mwezi kwan hata kama unaingiza milioni moja kwa mwezi na matumizi yako ni laki tisa na nusu kwa mwezi huwezi fanana na anaeingiza shilingi laki tano na matumizi yake kwa mwezi ni laki mbili kwa mwezi.
Wekeza pesa yako sasa katika biashara ili uje uwe na uhuru wa pesa zitakazokufanya utimize ndoto zako kwa sababu kama ukiogopa kuthubutu utakuja kuwatumikia wale walioamua kuthubutu.

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments system

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | coupon codes