Sunday, July 19, 2015

JE UNASUMBULIWA NA KISUKALI?


Miongoni mwa magonjwa sugu yanayoendelea kuathiri afya za mamilioni ya watu katika nchi nyingi duniani zikiwemo za bara la Afrika ni ugonjwa wa kisukari. Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni 285 wanasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari duniani ambapo karibu asilimia 90 ya wagonjwa hao wana aina ya pili ya kisukari. Jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa, idadi ya watu wenye kisukari inaongezeka kwa kasi na wataalamu wanasema kuwa, ifikapo mwaka 2030 idadi hiyo itaongezeka maradufu. Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wa kisukari katika nchi za Asia na Afrika, na inasemekana idadi hiyo inatokana na kukua miji na mabadiliko ya maisha ya watu katika nchi zinazoendele, na labda kutokana na kuiga mifumo ya maisha ya Kimagharib
Ugonjwa wa kisukari au Diabetes Mellitus hutokea pale tezi kongosho au pancrease inaposhindwa kutengeneza homoni au kichocheo aina ya Insulin, au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho cha insulin na kusababisha kuongezeka kiwango cha sukari kwenye damu au kitaalamu hyperglycemia. Insulin ni kichocheo au homoni inayotengenezwa na kongosho ili kudhibiti sukari katika damu. Ugonjwa wa kisukari unaweza kusababishwa kuwa na kiwango kidogo cha Insulin mwilini, mwili kutosikia kichocheo hicho au yote mawili.

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments system

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | coupon codes