Biashara Ya Mtandao- Mult-level Marketing
Ni mfumo ambao hutoa fursa kwa watu kujitengenezea kipato cha ziada ili kiwasaidie kufanya uwekezaji mkubwa bila kutumia mikopo kutoka katika taasisi za kifedha.
Mfumo huu ulianza mnamo mwaka 1920 huko Ausralia na badaye kusambaa dunia nzima.
Biashara hii humwezesha mtu kuendesha biashara yake kwa kutumia rasimali watu.
Mtaji wa biashara hii hauhitaji Milion wala Dhamana ya mkopo kutoka benki au taasisi nyingine za kifedha; Mtaji pekee wa biashara hii ni rasilimali watu wanaokuzunguka.
Nguzo Mama Katika Mfumo Wa Biashara Ya Mtandao
Watu:
Katika biashara hii ya mtandao rasilimali watu ndio msingi mkuu na mtaji pekee katika mafanikio biashara.
Biashara hii iliitwa biashara ya mtandao (Mult-level Marketing –“MLM”) si kwa sababu inafanyika kwa kutumia mitandao ya kiteknolojia kama vile Simu na Tanakilishi (kompyuta).
Iliitwa biashara ya mtandao kutokana na ushirikishwaji wa watu katika biashara, ambao hutengeneza mtandao wa kibiashara katika usambazaji na utumiaji wa bidhaa.
Hivyo dhana kubwa katika biashara hii ni kushirikiana na watu.
Kadri unavyokuwa karibu na watu na kuwashirikisha katika biashara yako ndipo unapotengeneza mtandao mkubwa wa kibiashara ( Business Network) ambalo ni bomba la pesa mfukoni mwako, kwani malipo huongezeka kulingana na mtandao wako wa kibiashara. Rasilimali watu ni utajiri katika MLM usiipuuze.
(The more the team you build; the long the pipeline of money into your pocket and the higher the sucess).
Muda:
Katika mafanikio yoyote muda ni muhimu sana.Hivyo katika biashara hii muda ni Mali Pesa. Ili uweze kufanikiwa katika biashara hii yakupasa kuwa mchumi katika matumizi ya muda wako.
Biashara hii inashirikisha watu, hivyo unahitaji kuwa na muda wa kuonana na watu ili kushirikishana juu ya biashara.
Biashara hii inahusisha bidhaa mbalimbali, hivyo unahitaji muda wa kupanga jinsi yakufanya manunuzi na kusambaza bidhaa zako.
Biashara hii inahitaji muda wa kujifunza na kuelekezana, hivyo unahitaji muda wa kuelekeza Watu wa timu yako na wanaotaka kujiunga na biashara.
Biashara ni ya kutengeneza timu ambao ndio mfumo wako wa kibiashara, unahitaji muda wa kufanya ufuatiliji wa timu yako ili kubaini matatizo ya mfumo wako, na kubainisha watu muhimu katika timu (Network) yako.
Biashara hii inahitaji malengo na mbinu mahusi za kufikia malengo, hivyo unahitaji mda wa kuchambua malengo yako ya kibiashara na kuweka mikakati jinsi gani ya kuyafikia.
Kadri unavyotumia mda wako vizuri katika biashara hii ndivyo unavyotengengeza ukubwa wa kipato chako. Kinyume chake ni sahihi.
Jitihada.
Hakuna mafanikio yoyote yanayopatikana pasipo kuwa na juhudi zozote; Mkulima ili apate mazao mengi lazima aweke juhudi katika kufanya kazi za shamba; Mwanafunzi ili afaulu lazima aweke juhudi katika masomo; Mfanyakazi ili aweze kuwa mfanyakazi bora lazima aweke juhudi katika kutimiza majukumu yake; Kadharika katika biashara ya mtandao, mafanikio pasipo juhudi ni sawa na kusubiri “kuvuna minazi kwenye shamba la migomba”. Ili ufanikiwe lazima uweke juhudi katika kutimiza majukumu yako ya kibiashara.
Weka juhudi katika kutengeza timu/mtandao wako wa kibiashara
Weka juhudi katika kuelimisha na kuwashirikisha watu juu ya biashara ya Mtandao
Weka juhudi katika kusambaza bidhaa zako
Weka juhudi katika kusaidia watu wengine wakue kibiashara
Weka juhudi katika kufuatilia mtandao wako ili kubaini matatizo ya timu yako
Weka juhudi katika kubaini changamoto za kibiashara na kutafuta ufumbuzi wake
Yote hayo kwa pamoja pasipo kuweka jitihada ni chanzo cha kutokufanikiwa katika biashara ya mtandao.
Katika biashara hii ya MLM: Watu + Muda + Jitihada = Mali Pesa
Mambo ya Kuzingatia kabla hujaanza Biashara ya mtandao
Kutokana na kushamiri kwa biashara hii, makampuni mengi yamejikita katika biashara hii kwani imeonekana kuwa yenye faida kubwa na yenye mfumo rahisi wa usambazaji bidhaa.
Hivyo kabla hujaanza kujiunga na biashara ya mtandao ni vyema kuzingatia yafuatayo ili uweze kuifanya biashara hii ya mtandao kwa ufanisi:
Tafuta Organization/ Kampuni iliyofanikiwa katika biashara.
Tafuta kampuni ambayo inafursa nyingi za kibiashara ambayo unaweza kushirikishana na watu wengine kwa urahisi.
Tafuta kampuni ambayo inamfumo mzuri wa Elimu ya biashara hii kwani Elimu ya biashara humfanya mtu kukua kibiashara na kuwa bosi wa biashara yake yeye mwenyewe na siyo mchuuzi wa bidhaa.
Tafuta kampuni ambayo inawatu wa uhakika unaowaheshimu, waliofanikiwa na ambao unafurahia kufanya nao kazi.
Tafuta kampuni yenye Viongozi wa kibiashara na siyo yenye Washauri ( Find the Campany that have strong mentors and not Advisors)
Tafuta kampuni yenye bidhaa bora; Mfumo mzuri wa malipo; mfumo Murua wa Usambazaji bidhaa na yenye bidhaa zinazoendana na kipato cha watumiaji wa aina zote.
Je wewe unataka kuwa mchuuzi au Mmiliki wa kibiashara?
Kwa wanaotaka kuwa wachuuzi wa bidhaa kabla hujajiunga na MLM unatakiwa kutumia mda mwingi kuangalia bidhaa na kutafuta wateja wa bidhaa hiyo huku jicho kubwa ukiangalia ubora
0 comments:
Post a Comment