Tuesday, July 14, 2015

MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA MKOJO NA UTATUZI WAKE

Maambukizi katika njia ya mkojo hujulikana zaidi kwa jina la UTI, kirefu chake ni Urinary Tract Infections.
Maambukizi haya tunaweza kuyaweka katika makundi makuu mawili:
(1) Maambukizi ya chini katika njia ya mkojo(lower urinary tract infections).
   Hii inahusisha mrija wa mkojo(urethra) na kibofu cha mkojo.
(2) Maambukizi ya juu katika njia ya mkojo(upper urinary tract infections.
  Haya ni maambukizi ambayo hupanda na kusababisha maambukizi kwenye figo.

Pia tunaweza kuchanganua ugonjwa huu katika namna kuu mbili.
(1) Acute UTI.
  Hii ni UTI ya kawaida tu. Haya ni maambukizi yanayoambatana na dalili zinzosababishwa na usumbufu wa maradhi kwenye njia ya mkojo. Kwa mfano kuumia wakati wa kukojoa, kukojoa mara kwa mara n.k.
(2) Chronic UTI.
  Hii mara nyingi huwa tunaiita UTI sugu. Katika hali hii huambatana na dalili za hatari kama kukojoa damu inayoweza kuonekana kwa macho tu bila msaada wa Microscope au kukojoa mkojo wenye chembechembe za damu nyekundu ambazo haziwezi kuonekana kwa macho. Sasa ukiona dalili hizo unaweza kujua kama una UTI sugu. Na unapofikia hali hii mara nyingi tunaamini kuwa tayari figo imeshambuliwa(pyelonephritis). Hapa ni kitendo cha kushambuliwa kwa kuta za nje za njia ya mkojo. Hapa mgonjwa anakuwa anasikia maumivu makali sana kwenye pingili za chini ya mgongo zikiambatana na dalili za tumbo kuuma chini ya kitovu na kukojoa mkojo wenye damu.

KWANINI WATU WENGI KILA KONA NI UTI?
Hii ni kwa sababu watu hawafuati utaratibu au kanuni za kuchukua vipimo maabara. Mfano kipimo cha UTI kwa Maabara tunapima kipimo cha mwanzo kwa kutumia mkojo wa katikati yaani MID STREAM URINE. Tatizo wengi wetu tukienda Hospitali tunaambiwa KAKOJOE HUMU ULETE MKOJO!
Mkojo wa mwanzo ni lazima upitie normal flora(bacteria rafiki/wasio na madhara), na kipimo cha mkojo huwa hakibagui, hapo ni lazima kitasoma una bacteria wengi kumbe wala siyo bacteria wenye madhara. Hapo inatakiwa ukojoe mkojo wa mwanzo umwagike kwanza ndipo uje uchukue mkojo unaofuata(wa katikati au mid stream urine catch).

WATU AMBAO WAPO HATARINI KUPATA UTI
=>Watoto wadogo wanaotumia Nepi maana wao hujikojolea humohumo. Hivyo mtoto mdogo kama humbadilishii Nepi mara kwa mara, huzinyooshi ili ziwe safi ana hatari ya kuugua UTI.
=>Wanaume wa umri mkubwa ambao hawajafanyiwa tohara.
=>Mwanamke yeyote yupo hatarini kupata UTI kwa sababu njia ya haja kubwa ipo karibu sana na njia ya uzazi. Na hivyo wengi wa wanawake wanapokuwa katika zoezi la kujisafisha hujisafisha kwa kupeleka uchafu mbele badala ya kusukuma huo uchafu kwa nyuma. Pia wanawake njia yao ya mkojo(urethra) ni fupi ukilinganisha na ya mwanaume. Kwa wanaume ni nadra sana bacteria kufika kwenye kibofu. Maambukizi ya kibofu huitwa CYSTIS.
=>Watu wenye wapenzi wengi yaani michepuko mingi na hawatumii kinga wakati wa kufanya mapenzi.
=>Wanawake wanaotumia nguo wakati wa kujihifadhi hedhi bila kuzikausha vizuri na kuzinyoosha. Kuna wanawake wengi hufua nguo na kuanika ndani nguo wanazotumia wakati wa hedhi.
=>Wanawake wanaotumia ped za madukani ambazo hazina viwango na kuchelewa kubadilisha ped.
=>Matumizi mabaya ya Antibiotics husababisha walinzi wa sehemu za siri kufa na kufanya bacteria nyemelezi kuvamia na kuanza kuharibu mazingira. Hivyo antibiotics ni nzuri lakini zitumiwe kwa misingi maalumu maana normal flora wakifa basi utashambuliwa na kila bacteria au fangasi ambao ni nyemelezi.

JE, VYOO VICHAFU NI CHANZO CHA UTI?
Watu wengi tumekuwa na visingizio kuwa bacteria wa chooni huwezi kuruka na kuingia katika via vya uzazi na kusababisha ugonjwa wa UTI. Ukweli ni kwamba hao bacteria hawana mabawa ya kuwafanya waruke ila sisi watu ndio huwa tunakiuka taratibu za kujisafisha tuwapo chooni. Kwa maana hiyo utaweza kuambukizwa UTI kupitia hivyo vyoo vichafu hasa vya jumuia endapo tu hautatumia Tishu zenye Antibiotics kujifutia.

SASA TUANGALIE TIBA YA UGONJWA HUU KWA KUTUMIA PED ZENYE ANIONS CHIP ZISIZO NA MADHARA.
Anions hizi zimewekwa katikati ya ped kwa kutumia pamba nyepesi. Hali hii huifanya sehemu husika ikilowa maji au damu, inafyonza damu yote na kuruhusu hewa kupenya na kusafisha joto lote kukausha unyevunyevu wote. Hewa inapopita inaondoa joto lote na kuondoa mazingira ya bacteria waharibifu kuweza kuota au kuishi maeneo hayo. Pia inasafisha na kukausha unyevunyevu wote ambao ukiachwa wadudu kama bacteria au fangasi huweza kuchekelea na kuzaliana kwa fujo. Hivyo kwa staili hiyo mwanamke au msichana unakuwa mkavu na hakuna joto kabisa kama vile kuna AC kwa jinsi utakavyojisikia mwenye amani.

SASA TUONE KAZI NA FAIDA YA HIZO ANION CHIP
=>Tujue kuwa hizo anions chip ni negative charged, yaani anions inapokuwa inatolewa inakuwa inatengeneza oxygen ambayo hii huzuia bacteria wote wanaoweza kustawi bila kuhitaji oxygen yaani Anaerobic Bacteria. Mfano mzuri ni mtu anayekuwa na kidonda cha anaerobes huwa kinanuka sana . Hivyohivyo harufu mbaya sehemu za siri kwa wanawake husababishwa na kuoteana kwa bacteria hawa. Hivyo kwa kutumia ped hizo hii hali huondoka kabisa.
=>Huzuia kansa ya shingo ya kizazi.
=>Hutibu kabisa UTI ya aina yoyote
=>Huzibua mirija ya uzazi kwa watu wenye matatizo ya uzazi
=>Huzuia harufu mbaya sehemu za siri
=>Inazuia maambukizi yote ya kizazi hasa unapokuwa katika mazingira hatarishi kama mabwawa ya kuogelea
=>Zinarekebisha tatizo la uwiano wa vichocheo au hormonal imbalances
=>Hurekebisha siku za hedhi kwa wanawake ambao siku zao za hedhi hubadilikabadilika.
=>Huondoa tatizo la kuumwa kichwa na tumbo wakati wa hedhi.

FAHAMU ZAIDI KUHUSU VIDOND VYA TUMBO N NAMNA YA KUJITIBU

Ugonjwa wa vidonda vya tumbo hutokea endapo kidonda cha ukubwa wa angalau nusu sentimeta kitatokea kwenye sehemu yoyote ya ukuta wa tumbo au utumbo wa binadamu. Kwa kawaida tatizo hili husababisha maumivu makali sana ya tumbo ingawa si lazima kila maumivu makali ayapatayo mgonjwa husababishwa na vidonda vya tumbo.

Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa karibu 70% - 90% ya vidonda vya tumbo husababishwa na vimelea vya bakteria wajulikanao kama HELICOBACTER PYLORI. Aidha matumizi ya baadhi ya dawa za kutuliza maumivu za jamii ya Non Steroid Anti-Inflamatory Drugs kama Aspirin au Diclofenac huweza kusababisha au kuongeza uwezekano wa kupata ugonjwa huu.

Kuna dhana iliyozoeleka kuwa vidonda vya tumbo huathiri zaidi mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo. Dhana hii si kweli kwani sehemu inayoathiriwa zaidi na tatizo hili ni sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo ijulikanayo kama Duodenum.

AINA YA VIDONDA VYA TUMBO.
1. Vidonda vinavyotokea katika mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo. Vidonda hivi hujulikana kama Gastric Ulcers.
2. Vidonda vinavyotokea katika sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo. Vidonda hivi hujulikana kwa kitaalamu kama Duodenal Ulcers.
3. Vidonda vinavyotokea katika koo (Oesophageal Ulcers)
4. Vidonda aina ya Merckel's Diverticulum Ulcers. Vidonda vya aina hii huweza kusababisha matatizo makubwa ya utumbo (intestinal obstructions)

CHANZO CHA VIDONDA VYA TUMBO
1. Maambukizi ya Bakteria aina ya Helicobacter pylor. Imeonekana kuwa zaidi ya 50% ya watu Duniani wana vimelea hivi katika utumbo. Aidha, miongoni mwao huwa hawaonyeshi dalili yoyote ya kuugua ugonjwa wa vidonda vya tumbo.
2. Matumizi ya muda mrefu ya dawa za kuondoa maumivu za kundi la NSAIDs. Ukuta wa utumbo hujilinda na madhara yatokanayo na tindikali ya utumbo (gastric acid) kwa kuwa na utando laini (mucus) ambao hutolewa na vichocheo vijulikanavyo kama Prostaglandins. Dawa hizi za kundi la NSAIDs huharibu mfumo wa utengenezaji vichocheo hivi yaani Prostaglandins na hivyo kufanya kuta za tumbo kukosa utando wa kuzilinda na mashambulizi ya tindikali hali ambayo hupelekea kutokea kwa vidonda vya tumbo.
3. Vyakula au viungo vya vyakula vyenye uchachu. Kinyume na ilivyozoeleka kwa wengi, baadhi ya vyakula vyenye uchachu na upilipili kama pilipili, ndimu, limao na masala havina uhusiano na uwezekano wa kupata vidonda vya tumbo.
4. Uvutaji wa sigara. Uvutaji wa sigara sambamba na maambukizi ya bakteria aina ya Helicobacter pylor huongeza madhara ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo. Ifahamike kuwa uvutaji wa sigara pekee hautoshi kusababisha vidonda vya tumbo isipokuwa kwa kushirikiana na bakteria wa Helicobacter pylor.
5. Watu walio katika kundi la damu la O. Imeonekana pia kwamba kundi la damu la BLOOD GROUP O, halina uhusiano wa kusababisha vidonda vya tumbo.
6. Unywaji wa pombe. Unywaji wa pombe kwa kushirikiana na bakteria wa Helicobacter pylor huongeza madhara ya vidonda vya tumbo.
Vitu vingine vinavyohusishwa na uongezaji wa ugonjwa wa vidonda vya tumbo ni pamoja na Upasuaji wa tumbo (major abdominal surgeris), kuungua kwa moto (burns), ugonjwa wa figo na kubadilishiwa kwa viungo vya mwili kama figo au ini.

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
-Maumivu makali au kiungulia maeneo ya chembe moyo (epigastric pains).
-Maumivu makali kipindi cha kula au baada ya kula.
-Maumivu makali wakati unapokuwa na njaa.
-Kuvimbiwa au tumbo kujaa gesi. Hali hii yaweza kuendana pamoja na kubeua au kujamba mara kwa mara.
-Kucheua au kuongezeka kwa mate yanayoshuka tumbomi baada ya kucheua.
-Kichefuchefu na kutapika.
-Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito.
-Kutapika damu.
-Kupata haja kubwa ya rangi nyeusi au kahawia chenye harufu mbaya sana. Hii humaanisha kuwa mgonjwa anapata haja kubwa au choo kilichochanganyika na damu kwa mbali.
Uwepo wa dalili kama kiungulia cha muda mrefu, kucheua na kutapika baada ya kula na historia ya kutumia  dawa za kupunguza maumivu NSAIDs kwa muda mrefu bila kufuata ushauri wa Daktari ni ishara moja ya kumfanya mgonjwa kumuona Daktari kumpima na kumfanyia uchunguzi ili kujiridhisha kuwa hana tatizo la vidonda vya tumbo.

MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO
Mara nyingi mchanganyiko wa dawa za Antibiotics mbili hasa Amoxyllin + Metronidazole sambamba na dawa yoyote ya jamii ya PPI kama Pantoprazole au Omeprazole. Hiyo ni kwa mgonjwa wa vidonda ambavyo siyo sugu.
Vidonda sugu inampasa mgonjwa kutumia dawa za antibiotics za aina tatu kama Amoxyllin + Clarithromycin + Metronidazole ambazo hutumika sambamba na dawa yoyote moja kutoka kundi la PPI kama Omeprazole na Pantoprazole pamoja na Bismuth Compound.

Iwapo hakuna ushahidi wa kuwepo kwa uambukizi wa bakteria, dawa yoyote moja ya jamii ya PPI yaweza kutumika kwa muda mrefu bila kuchanganya na antibiotic yoyote.
Hata hivyo inawezekana kabisa ugonjwa huu kujirudia, hivyo ni vyema kuhakikisha unapata matibabu sahihi na uhakikishe unamaliza dozi kwa muda sahihi. Kumekuwa na watu wengi kuanza matibabu vizuri lakini huishia njiani na kutomaliza dozi. Huu siyo ugonjwa mdogo kwamba utumie dawa kwa siku tatu au wiki moja kisha unapona, huu ni ugonjwa sugu hivyo matibabu yake pia ni ya muda mrefu kidogo kutegemeana na aina ya dawa unazotumia.
Dawa iliyotengenezwa kwa mmea wa Mwalovera imekuwa msaada mkubwa kwa wagonjwa wote wa vidonda vya tumbo. Hutibu kabisa vidonda vya tumbo kwa kuwaangamiza kabisa bakteria wote wasiofaa katika tumbo. Dozi tatu za dawa hii kwa muda wa miezi mitatu humaliza kabisa ugonjwa huu.
=>Kuipata dawa hii wasiliana nasi kwa 0767925000 au 0784925000 utaweza kuipata mahali popote ulipo.

Wednesday, July 1, 2015

SCHOOL DID'NT TRAIN YOU TO BE BUSINESS OWNER IT TRAINED YOU TO BE IMPLOYED FOR RICH.

Hellow wapendwa natumaini wote mu wazima na kwa wale ambao hampo sawa poleni na naamini Mungu atawapa uponyaji.Siku ya leo nimependa tujifunze ni jinsi gani mfumo wa elimu ambavyo unatujenga tuwe wategemeaji kwa kutujenga kuja kuajiriwa na sio kujiajiri sisi wenyewe.
Katika mfumo wa elimu Tanzania na duniani kwa ujumla hakuana mtaala unaomjenga mtu kuja kujiajiri mwenyewe bali unamtengenezea mwanafunzi mazingira ya kuja kuajiriwa,kwa mfano,nilikutana na mwanafunzi aliyehtimu shahada ya kwanza biashara akilalamika katafuta kazi bila mafanikio,nilipomuuliza kwani huwezikwa kutumia elimu uliyonayo juu ya biashara kujiajiri mwenyewealidai tatizo ni mtaji.Hapo ndipo nilipogundua kumbe hata wanaosomea biashara wapo sawa kama waliosomea shahada nyingine.
Mfumo wa elimu haumfundishi mwanafunzi kuja kujiajiri bali unamfundisha mtu kuja kuwatumikia matjiri(wafanya biashara),kwa mfano unakuta mtu kasomea uhandisi ila kaajiriwa katika kampuni la uhandisi la mfanyabiashara aliyeishia form four,na anafurahia hiyo kazi kwa kuona analipwa kipato kikubwa bila kujua kwamba yeye anamuingizia mara themanini au tisini mwajiri wake.
SIku hizi wafanyabiashara wakubwa kama kina Bakhresa wanawatumia wasomi kwa kununua projects proposal mbali mbali na kuzifanyia kazi zinazowaingizia mabilioni ya pesa na unakuta aliyeiuza hiyo proposal anafurahia kisa amaelipwa milioni ishirini au thelasini.
Mafanikio ya mtu yanaangaliwa katika pesa na jinsi gani anatumia akili yake katika kukikuza kipato chake,hapa haijarishi kichwani kwako umebeba degree ngapi,unakuta mtu anapata fursa ya kufanya biashara anadai hawezi ichafua degree yake kwa kufanya biashara za kijinga wakati kina pinda na uwaziri wao wanawekeza mpaka mashambani ambapo ndio panaonekana pa walala hoi.Tumia elimu uliyonayo kukikuza kipato chako,hata kama unaajira usitegemee utakaa kwenye ajira miaka yote siku utakapoishiwa nguvu hajkuna atakayeangalia umesomea chuo gani wala nchi gani kwa sababu hautakua na faida yeyote,na kama unasubiria pensheni ndio ikutajirishe unajidanganya kwasababu nguvu unayoitumia inatengebneza mamilioni ya pesa kwa mwajiri wako na hiyo pesheni yako ni vijisenti tu katika rundo la pesa ulilotengeneza.
Kuanza biashara haijarishi una shilingi ngapi mfukoni kwani unaweza izalisha shilingi hamsini uliyonayo ikawa mia,elfu na mwisho wa siku ukawa mfanya biashara mkubwa,kuwa tajiri haijarishi kiasi kiasi kikubwa cha pesa unachotengeneza kwa mwezi bali unawekeza kiasi gani cha kipato chako katika miradi.
BONIVENTURE JOACHIM

Kongamano

Biashara

Boni

Disqus Shortname

Comments system

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | coupon codes